Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, August 14, 2018

Mbosso Amjibu Rich Mavoko kuhusu WCB kuwanyonya wasanii

Msanii wa Bongo Fleva, Mbosso amesema haamini iwapo WCB inawanyonya wasanii.

Muimbaji huyo akipiga stori na SnS Tanzania (Simulizi na Sauti) amesema kwa upande wake anaamini fedha iliyowekezwa kwake haijarudi, hivyo hawezi kuona iwapo ananyonywa.

"Nilipoingia WCB hadi kufikia leo nahisi bado sijarudisha  pesa ambayo wamewekza kwangu, kwa hiyo nikiambiwa nanyonywa binafsi nitapiga kwa sababu naona mimi ndio nawanyonya hadi leo kuna baadhi ya hela imetumika kwangu haijarudi.

"Na ukifanya masihara kuna wasanii wengine wamo mule mule hela ambayo imetumika kuwafanyia brand haijarudi, kwa hiyo ikija ukaniambia Mbosso unanyonywa WCB toka uje na vigezo, uje na ushahidi wa kutosha kwamba nanyonywaje," amesema Mbosso.

Kauli ya Mbosso inakuja mara baada ya hivi karibuni kuripotiwa kuwa msanii Rich Mavoko amepeleka mkataba wake na WCB kwenda kupitiwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kwa kile kinachodaiwa kuwa ulikuwa wa kinyonyaji.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )