Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, August 26, 2018

Mbossoa Akana Kunyonywa na WCB

Msanii kutokea WCB, Mbosso amesema hadi sasa fedha iliyotumika na lebo hiyo kwenye kazi zake haijarudi, hivyo hawezi kusema ananyonywa.

Muimbaji huyo kwenye mahojiano na The Playlist ya Times FM amesema suala la kunyonywa kwake na WCB halipo kabisa.

"Mimi leo hii nikisema nanyonywa , nitakataa kabisa kwa sababu nikijiangalia Mbosso wa mwaka jana hadi sasa najiona nimesogea hatua kubwa sana," amesema.

"Ukiachilia hilo mimi naona kama nawanyonya wao  kwa sababu hadi leo naweza kusema pengine pesa walizowekeza kwenye kazi zangu hata nusu yake sijairudisha bado," amesema Mbosso.

Alipoulizwa ni ushauri gani anaukumbuka kutoka kwa Rich Mavoko, alijibu; "Kuna siku alishaniambia kuhusu kurekodi nyimbo tu, akaniambia ili uwe msanii mzuri hakikisha nyimbo zilizoko ndani ni nyingi kuliko zilizotoka,".
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )