Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, August 14, 2018

Mbunge wa CHADEMA Anthony Komu Akanusha Taarifa za Kutaka Kuhamia CCM

adv1
Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini (CHADEMA), Anthony Komu amekanusha kauli iliyotolewa na aliyekuwa Mbunge wa Ukonga (CHADEMA) kuwa mbunge huyo yuko mbioni kutimkia CCM.

Komu amesema kuwa hawezi kuondoka CHADEMA na hajawahi kufanya mazungumzo na Waitara kuhusu suala hilo kwani yeye ndio muasisi wa upinzani na anajivunia historia hiyo .

“Mimi sio sehemu ya mpango huo na sielewi Waitara katoa wapi taarifa hiyo naomba wananchi wangu watambue kuwa mimi sio mpinzani wa kuunga unga mimi ni miongoni mwa waasisi wa upinzani”, amesema Komu.

Jumamosi ya Agosti 11, 2018 wakati akiongea na kituo cha EATV,  Waitara aliwataja wabunge watano kutoka CHADEMA wanaotaraji kujiunga na CCM akiwemo Anthony Komu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )