Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, August 14, 2018

Meli ya mizigo yawaka moto bandari ya Bagamoyo

adv1
Meli mali ya kampuni ya Ocean Enterprises Limited ya Zanzibar imeungua moto wakati ikiwa imeegeshwa kwenye ufukwe ya Bahari ya Hindi huko Bagamoyo mkoani Pwani.

Tukio hilo limetokea leo saa 12.15 asubuhi  wakati meli hiyo ikiwa imepaki kwenye fukwe hiyo kwa ajili ya kupakia mizigo mbalimbali ikiwemo saruji zilizokuwa zikisafirishwa  kwenda visiwani Zanzibar.

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto kituo cha Bagamoyo Iward Mwanza amesema wamepokea taarifa ya moto huo saa 12.24 asubuhi na askari walifika saa 12.30 eneo la tukio.

"Ni kweli moto ulizuka kwenye hii meli na tulipata taarifa asubuhi saa 12.24 hivi tukajipanga na kufika bandarini tukakuta sehemu ya mbele ilikuwa imeshashika moto na ulikua ukiendelea kusambaa melini,”amesema.

Amesema walianza kuudhibiti ili usilete hasara zaidi na walifanikiwa. Mkuu huyo wa zima moto Bagamoyo amebainisha kuwa uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )