Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, August 3, 2018

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya TWAWEZA Adai Kunyang'anywa Paspoti

adv1
Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan  Eyakuze, amesema Idara ya Uhamiaji inashikilia hati yake ya kusafiria tangu Julai 24, ambapo pia licha ya kuwa na hati ya dharura, juzi Agosti Mosi mwaka huu alizuiliwa kusafiri kwenda jijini Nairobi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Agosti 3, Eyakuze amesema aliitwa uhamiaji na kutakiwa kupeleka hati yake ya kusafiria bila kuwa na taarifa yoyote ya amri ya kimahakama yenye kuidhinisha jambo hilo.

“Niliitwa Uhamiaji nikahojiwa kidogo na kuambiwa nipeleke pasipoti yangu sikuona haja ya kukataa sababu ni haki yao kuchukua, ila hadi sasa sijapata tamko rasmi kwa nini wamechukua,” amesema.

Aidha, Mkurugenzi huyo amesema Twaweza wataendele kufanya kazi zao kama kawaida pamoja na changamoto wanazopitia, ikiwamo kutumiwa barua mbili na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), ikiwahoji kuhusu uhalali wa programu yao Sauti za Wananchi na kuwataka wafafanue kwanini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yao.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )