Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, August 6, 2018

Mtoto Abakwa Na Kusababishiwa Fistula

Mwanafunzi  wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka minane mkoani Manyara, anadaiwa kubakwa na mkazi mmoja wa wa Kijiji cha Maganjwa wilayani Babati na kumsababishia   ugonjwa wa fistula.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Dareda,  Joseph Lorri,  alithibitisha kupokewa mtoto huyo ambaye alikuwa na hali mbaya ikiwamo kuvuja damu kutokana na majeraha ya kuchanika sehemu za siri ikiwamo haja ndogo na kubwa.

Alisema mtoto huyo alipokewa hospitalini hapo Julai 16, mwaka huu saa 3.30 usiku akiwa ameharibiwa sehemu zake za siri na anavuja damu na kutokwa nyama sehemu zake za  siri.

“Tukio lenyewe linavyoelezea mtoto huyu alibakwa, na mtoto alimtaja aliyembaka ambako jamii ilikuwa ikimtafuta mbakaji huyo.

“Alivyoletwa alikuwa anatoka damu sehemu za siri na kulikuwa na mpasuko wa kidonda  kwenye sehemu ya haja kubwa na ndipo tukaanza kumfanyia vipimo,” alisema Dk. Lorri.

Alisema mtoto huyo alitibiwa kwa kufanyiwa upasuaji  na kushonwa kuunganisha sehemu hizo zilizochanika na kwamba hadi sasa hali yake inaendelea vizuri kwa uangalizi wa madaktari wa hospitali hiyo.

“Tunaendelea na jitihada za kumtibu lakini pi tumemwanzishia matibabu ya dawa za kumkinga dhidi ya maambukizi ya virusi  kutokana na tukio lenyewe jinsi lilivyokuwa,” alisema

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )