Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, August 23, 2018

Polisi Wanaowabambika Kesi Raia Wazidi Kubanwa

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ameendelea kuwabana polisi akiwataka kuachana na tabia ya kubambikia raia kesi zikiwamo za uzururaji na ugaidi.

Lugola alitoa kauli hiyo Jumatatu jioni baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Chuo cha Taaluma cha Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam na kuzungumza na maofisa wa chuo hicho na wanafunzi.

Alisema aliamua kufanya ziara hiyo baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa raia kuhusu kubambikwa kesi na askari polisi.

"Miongoni mwa kesi ambazo raia wanalalamikia kubambikiwa sana ni uzururaji na kesi za ugaidi," Lugola alisema.

Waziri huyo aliongeza kuwa, kuna maofisa wenye vyeo ndani ya jeshi hilo aliokutana nao lakini kutokana na vitendo vyao amewatilia shaka kama kweli waliwahi kupitia mafunzo chuoni hapo.

"Kuna baadhi ya mambo yanayofanyika kule chini ambayo yananishangaza sana, nimekuwa nikijiuliza jeshi hili ni la weledi na wa kisasa kweli? Yuko OCS mmoja (Mkuu wa Kituo) kama ninyi, yupo kwenye kituo cha polisi.

"Yeye kila kukicha asilimia 90 ya watu ambao anawakamata na kuwaweka ndani wote ni dili analotengeneza yeye, najiuliza ina maana siku hizi tunakwenda kusoma tuje kutengeneza madili?"

"Moyo wa kufukuzia madaraka haupo, nimeona umuhimu wa mafunzo haya pengine mimi nikisema mtabadilika na ninyi wakati mnasoma mtakuja kunikumbuka siku moja kuwa alikuja waziri akatukumbusha.

"Si lazima uchafuke mabega upate madaraka, kuna watu wamechafuka mabega lakini ndiyo hao wa madili... kuna watu hawajachafuka wanafanya kazi vizuri, wapo huko vituoni."

Waziri huyo aliwataka maofisa na askari chuoni hapo kuhakikisha wanatumia mafunzo hayo kulinda usalama wa raia na siyo kuwakandamiza kwa kuwabambikia kesi mbalimbali.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )