Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, August 1, 2018

Rais Magufuli Awataka Viongozi wa Jiji la Dar es Salaam Wajitafakari

Rais John Magufuli, amewataka viongozi wa Jiji la Dar es salaam,  kujitafakari katika utendaji kazi wao kwani imeonekana kukwama katika sekta mbalimbali ikilinganishwa na majiji mengine.

Kauli hiyo ameitoa leo katika hafla ya uapishwaji wa viongozi walioteuliwa wakiwamo Wakatibu wa Wakuu wa wizara mbalimbali, Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala iliyofanyika Ikulu jijini.

Rais Magufuli amesema kumekuwa na ‘upigaji’ mkubwa huku viongozi wakiangalia bila kuchukua hatua zozote.

“Juzi nilikuwa naongea na mabalozi, nikawaambia Dodoma ndiyo inaongoza katika majiji, manispaa, wilaya Tanzania nzima hivyo unaweza ukajiuliza kuna nini unaweza ukajua hapa Dar es salaam kuna upigaji na viongozi wapo,” amesema Magufuli.

Amesema viongozi wa Dar es salaam wakikutana kwenye vikao wanakaa siku mbili lakini zitajazwa ni siku nne hivyo kwa namna hiyo hawawezi kupata mapato kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

“Utakuta hata wamachinga wanasimama barabarani hawana mahali pa kufanyia biashara, wakina mama wamedhulumiwa lakini viongozi wapo hivyo nataka niwaambie viongozi mlioteuliwa hakuna mwenye garantii ya kazi,” amesema Rais Magufuli.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )