Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, August 8, 2018

Rc Makonda Atembelewa Na Rais Wa TFF

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana ametembelewa ofisini kwake na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Wallace Karia na Mwenyekiti wa Michezo Mkoa wa Dar es Salaam ambapo wamefanya mazungumzo ya kuimarisha sekta ya Michezo.

Miongoni mwa mambo waliyozungumzia ni Suala la heshima iliyopata Tanzania kuwa mwenyeji wa Michuano ya Mashindano makubwa ya michezo kwa Jeshi la Polisi katika nchi za mashariki na Kati zikihusisha Nchi Saba ambapo tayari michuano hiyo imefunguliwa rasmi  na Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

Aidha wamezungumzia maandalizi ya mashindano makubwa ya SECAFA Cuf kwaajili ya michuano ya AFCON yakihusisha vijana wenye umri chini ya miaka 17 yanayotaraji kufanyika August 11 Mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa yakijumuisha mataifa 10 Afrika.

RC Makonda amesema michuano yote hiyo itafanyika Jijini Dar es salaam na kwakuwa inahusisha ugeni kutoka mataifa mbalimbali itatoa fursa kwa wananchi wa Dar es salaam hususani wenye hotel, vyakula, usafiri na wafanyabiashara kupata kipato kupitia mashinano hayo.

Kwa upande wake Rais wa TFF Wallance Karia amempongeza RC Makonda kwa jitiada za kuinua sekta ya michezo kupitia ujenzi wa uwanja wa Bandari ambapo amesema wameamua kumuomba ushirikiano kwakuwa wanaamini uwezo ukubwa alionao kwenye kusimamia jambo na kufanikisha.
 
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )