Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, August 4, 2018

Roma Ajibu Kuhusu Kuonekana na Wema Sepetu Hotelini

Msanii wa muziki Bongo, Roma amefunguka kuhusu taarifa za yeye kufanya video na  Wema Sepetu.

Rapper huyo katika mahojiano na The Playlist ya Times Fm amesema kuwa walikutana hotelini kwa ajili ya kupata chakula cha mchana ndipo wakapiga picha na hakukuwa na zaidi ya hapo.

"Hiyo stori ya Wema nilikutana naye nilikuwa naenda Ivan (jina la hoteli) kula lunch, kwenye moja na mbili tukawa tunapiga naye stori ndiyo hizo picha zikaja lakini hamna chochote, sio mchongo wa chupa wa video, ni familia tu," amesema Roma.

Kwa sasa Roma na Stamina (Rostam) wanafanya vizuri na wimbo wao mpya uitwao Parapanda mara baada ya kufanya vizuri na ngoma kama Hivi Ama Vile pamoja na Kiba_100.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )