Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, August 16, 2018

Serikali Yatahamaki Saruji Kuadimika Sokoni na Kupanda Bei....Yawaita Wadau Kujadiliana

Serikali imekutana na wadau wa sekta ya viwanda kujadili kuadimika kwa saruji, huku inayopatikana ikiuzwa bei ya juu.

Kikao hicho kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya kilihudhuriwa na wazalishaji wa saruji na wa makaa ya mawe, wasafirishaji na wadhibiti.

Akizungumza katika mkutano huo Manyanya amewataka wazalishaji wa saruji kueleza uwezo wao wa uzalishaji.

Naibu waziri pia amewataka kueleza sababu za kusimamisha uzalishaji ghafla na kwa viwanda vyote.

"Imetushitua kuona saruji imepotea sokoni na kupanda bei ghafla, tena viwanda vyote. Tukasema hapo ni zaidi ya masuala ya kiufundi, kwa hiyo tumewaita kuwasikiliza tujue tatizo ni nini ikiwezekana leo tutoke na uamuzi,” alisema Manyanya.

Alisema sasa kuna fursa nyingi za soko la saruji kupitia miradi inayotekelezwa na Serikali na kwamba  hiki ndicho kipindi cha kuongeza uzalishaji lakini anashangazwa kuona saruji imeadimika na bei imepanda.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )