Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, August 13, 2018

Twaweza Yakanusha Habari Ya Gazeti La Tanzanite Iliyodai Mkurugenzi Wake Ni Mwanachama Wa Chadema

Taasisi ya Twaweza imekanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti la Tanzanite  kuwa Mkurugenzi wake, Aidan Eyakuze ni mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Aidan Eyakuze si mwanachama wa Chadema na hajawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini.

Hata hivyo, Wameongeza kuwa Twaweza ni taasisi huru isiyofungamana na chama chochote cha kisiasa hivyo taarifa iliyoandikwa na gazeti hilo ni ya uongo

==>>Isome taarifa yao hapo chini
 Twaweza imeona taarifa za uongo kwenye gazeti mojawapo la Agosti 13, 2018. Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza sio mwanachama na hajawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini Tanzania.

Twaweza ni taasisi huru isiyofungamana na chama chochote cha siasa. Tunaamini katika uhuru na haki za msingi ikiwemo uhuru wa kujumuika na uhuru wa kutoa maoni. 

Hizi ni haki za msingi za binadamu ambazo zimeainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Mitazamo ya kisiasa au uanachama wa kisiasa wa mfanyakazi yeyote wa Twaweza haushawishi maudhui ya kazi zetu na tafiti tunazochapisha.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )