Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, August 4, 2018

Updates: Kingwangalla Kwa sasa Yuko Hospitali ya Muhimbili

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amewasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.

Ndege iliyombeba waziri huyo ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12 jioni, msafara kuondoka kuelekea Muhimbili.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya na mkurugenzi mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru pamoja na jopo  la madaktari wamempokea Dk Kigwangalla katika  kitengo cha magonjwa ya dharura Muhimbili.

Dk Kigwangalla amepata ajali leo Jumamosi Agosti 4, 2018 eneo la Magugu mkoani Manyara na kupata majeraha sehemu mbalimbali mwilini

Awali,  waziri huyo alipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Magugu na kuhamishiwa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center kwa helkopta.

Katika ajali hiyo ofisa habari wa wizara hiyo, Hamza Temba amefariki dunia.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )