Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, August 28, 2018

VIDEO: Waziri wa Fedha Dr. Mpango Alivyopangua Laana za Makonda

adv1
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ameagiza makontena 20 ya samani yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yapigwe mnada ikiwa ni sehemu ya kusimamia sheria na kanuni za kodi zilizopo nchini.

Ametoa maagizo hayo jana  jijini Dar es salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kwenye Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na kukagua makontena hayo katika Bandari Kavu ya (DICD).

Aidha, Waziri Mpango ameweka wazi kwamba hajali vitisho vya mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam na ameapa kuendelea kusimamia sheria na kanuni za kodi nchini na hilo halichagui mtu wala nafasi yake.

Akiwa kwenye ibada jana huko Wilayani Ngara mkoani Kagera, Paul Makonda alitoa onyo kwa mtu atakayenunua makontena hayo  yenye samani za ndani kama vile meza, viti na mbao za kufundishia  kuwa atapata laana yeye pamoja na kizazi chake chote.

==>>Msikilize hapo chini Dr Mpango akizipangua hizo laana
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )