Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, August 8, 2018

Walichoongea Rais Magufuli na Viongozi wa Dini Baada ya Kukutana Jana

Rais John Magufuli  jana alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa dini za kikristo nchini { Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)}. Katika mazungumzo yao Rais amewataka kufanya kazi na kuendelea kuhubiri kuhusu amani, upendo na mshikamano.

“Nawahakikishia mimi nipo pamoja na nyinyi, nendeni mkafanye kazi kwa kujiamini na kwa uhuru, mkiwa na jambo lolote nijulisheni nitalishughulikia, wahubirieni Watanzania amani, upendo, mshikamano na kuipenda nchi yao,” alisema Rais Magufuli.

Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa  Rais  alikutana na kujadilina na viongozi hao kuhusu ushirikiano.

Rais Magufuli amewashukuru kwa dhamira yao ya kutaka kukutana nae na kufanya naye mazungumzo na amewahakikishia kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa madhehebu ya dini na taasisi zake.

Amesema serikali itaendelea kushirikiana nayo katika kuwahudumia na kuwaletea maendeleo wananchi.

 Anaeleza katika mazungumzo hayo viongozi hao wamemhakikishia utayari wao wa kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Serikali, kuyasimamia makanisa yao ili yaendelee kutoa huduma ya kiroho na kijamii kwa manufaa ya Watanzania wote na kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazojitokeza.

Pia viongozi hao wamempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya wamu ya tano katika kuleta maendeleo na kuimarisha huduma za kijamii ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya usafiri na majengo, kuleta nidhamu katika utumishi wa umma, mapambano dhidi ya rushwa.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )