Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, August 12, 2018

Waziri Kairuki Awapa Angalizo Wafanyabiashara wa Madini

WAZIRI wa Madini, Angella Kairuki amewataka wafanyabiashara wa madini nchini wazingatie sheria, kanuni na taratibu kwa kufanya biashara halali ili kuziwezesha pande zote yaani serikali na wafanyabishara kunufaika na rasilimali hiyo.

Amesema hayo jana wakati akizungumza na wafanyabiashara wa madini wa jijini Arusha waliohudhuria mkutano huo ulioratibiwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA).

Kairuki amesema zama zimebadilika na hivyo kuwatahadharisha wale wote wanaofanya vitendo vilivyo kinyume cha taratibu na kueleza kuwa, hawatasalimika na mkono wa sheria kwa kuwa serikali imedhamiria kuhakikisha kwamba rasilimali madini inawanufaisha Watanzania na Taifa.

Amesisitiza kuwa, tayari ana taarifa za kila mfanyabiashara wa madini wa jijini Arusha na kuwataka wote wanaokwenda kinyume kujitafakari upya na kuchukua hatua sahihi kwani anamfahamu kila mmoja.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )