Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, August 27, 2018

Waziri Mkuu Mgeni Rasmi mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano wa 14 wa mwaka wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) utakaofanyika kesho jijini Dar es 
Salaam.


Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye,
maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na utatanguliwa na mkutano mwingine wa wajumbe kutoka kongani 14 zinazounda sekta binafsi.

"Mkutano huo ni muhimu sana kwani ndiyo utakaotoa nafasi kufanya uchaguzi wa wajumbe 14 wa bodi ya wakurugenzi ya TPSF wajumbe hao ndiyo
watakaopendekeza majina mawili ya wagombea wa nafasi ya mwenyekiti wa taasisi hiyo," alisema Simbeye.

Simbeye alieleza kuwa wajumbe 14 kutoka kila kongani watakaochagulia na kuidhinishwa kwa
kawaida huwa pia ni wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) wakiungana na wajumbe wengine 14 kutoka sekta ya Umma ambapo Rais ndiye mwenyekiti wa Baraza.

Alisema maudhui ya mkutano huo ni ‘Uongozi, biashara unaowajibika katika ushirikiano wa sekta za umma na binafsi kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi’.

Alisema wajumbe watakaochaguliwa kwenye mkutano huo watatangazwa na kuridhiwa na mkutano wa mwaka na kwamba majina mawili yatakayopendekezwa yatachaguliwa kwenye nafasi za mwenyekiti na makamu mwenyekiti.

"Katika bodi inayomaliza muda wake, Mwenyekiti alikuwa Dk. Reginald Mengi na Makamu Mwenyekiti alikuwa Salumu Shamte ambao wamefanya kazi nzuri ya kuiimarisha sekta binafsi nchini," alisema Simbeye.

Simbeye aliongeza kuwa mikutano na vikao mbalimbali ambavyo vimefanywa kati ya sekta za umma na binafsi chini ya bodi inayomaliza muda wake vimekuwa na mafanikio makubwa.

Pia alisema Novemba 20, mwaka huu TPSF itaadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake.

Aliongeza kuwa TPSF ipo mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za Serikali ya Rais John Magufuli.

“Sisi sekta binafsi tumejipanga kutokomeza vitendo vya rushwa miongoni mwa wanachama wetu. Kuimarisha uhusiano wetu na serikali ikiwamo kuhamasisha ulipaji wa kodi miongoni mwa wanachama wetu pia," alisema Simbeye

Jumuiya zinazounda TPSF zinajumuisha Kilimo, Viwanda, Utalii, Benki na Fedha, Madini,Huduma, Wanawake Wajasiriamali, Wafanyabiashara Zanzibar, Ujenzi na Uhandisi, Mafuta na Gesi, Usafirishaji, Makampuni, Biashara na Uchuuzi.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )