Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, August 16, 2018

WCB waeleza bado Rich Mavoko ni wao, na hakuna Mkataba wa Kinyonyaji

adv1
Meneja Sallam SK kutokea WCB amesema hadi sasa Rich Mavoko ni msanii wao licha ya yote yanayozungumzwa.

Katika mahojiano na The Playlist ya Times FM amesema bado anashindwa kuelewa malalamiko ya msanii huyo ni yapi kwa sasa,

"Rich Mavoko mpaka sasa ni msanii wa WCB;  Nasema ambapo ni mkataba ulivyo, Rich Mavoko ni msanii wa WCB na pato lake lote linapitia WCB," amesema.

Ameendelea kwa kusema hata channel ya YouTube ya msanii huyo aliyopandisha wimbo wake mpya 'Happy' ipo chini ya WCB.

Pia ameeleza kuwa iwapo ameamua kujitenga na wenzake ni maamuzi yake kwani huwezi kumpangia mtu ila bado wanatambua ni msanii wao na hajawahi kupewa adhabu ya kusimamishwa kama inavyodaiwa.

"Mpaka sasa hivi sijui malalamiko yake ni yapi kwa sababu ukisema sisi tunamnyonya mtu hiki kitu hakiwezekani. Kwanza ukiangalia kwenye mkataba wetu msanii anapata percent kabla hajakatwa kodi, ukiangalia hapo nani ananyonywa?," amesema Sallam SK.

Utakumbuka August 09, 2018 msanii Rich Mavoko alifika ofisi za Baraza la Sanaa Taifa, moja ya vitu vilivyoelezwa ni kuwa alipeleka mkataba wake na WCB katika Baraza hilo kwa kile kinachodaiwa ulikuwa wakinyonyaji.

Mkataba huo inatarajiwa kupitiwa na Tume uliyoundwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ingawa  BASATA walieleza kuwa kutakuwa na kikao kati ya WCB na upande wa Rich Mavoko kwa lengo la kusuluhisha.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )