Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, August 19, 2018

WCB wafunguka ishu ya Rich Mavoko kujisajili upya BASATA

WCB imesema taarifa za Rich Mavoko kwenda kujisali Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) si sawa kwani tayari alikuwa ameshasajili kupita lebo hiyo mwaka huu.

Meneja kutokea WCB, Sallam SK amesema hayo alipokuwa akieleza ushirikiano uliyipo kati ya WCB na Baraza hilo kwa sasa.

"Suala la kusema hatushirikiani na BASATA hilo litakuwa si la kweli na sisi tunashirikiana nao sana kuna vitu vinatokea bahati mbaya. Lakini ukiangalia wasanii wetu wote wamesajiliwa BASATA na hamna yeyote ambaye hajawahi kujisajili," amesema.

"Hata juzi kati hapa ilisemekana kuwa Rich Mavoko ndio alienda BASATA akajisajili, hapana!, kashasajili kupitia WCB, actually mwezi wa saba mwaka huu," Sallam SK ameiambia The Playlist ya Times FM.

August 09, 2018 msanii Rich Mavoko alifika BASATA kwa kile alichoeleza alienda kujisajili na Baraza hilo lilithibitisha hilo pia.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )