Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, September 19, 2018

Baba Levo Kaachiwa Huru na Mahakama

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma imemuachia huru diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini (ACT-Wazalendo), Crayton Revocatus ‘Baba Levo’.

Baba Levo ambaye ni msanii wa Bongo Fleva alikuwa anakabiliwa na mashtaka matatu ya kushambulia, vurugu na lugha ya matusi dhidi ya muuguzi wa zahanati ya Msufini, Christina Gervas.

Akisoma hukumu hiyo leo Jumatano Septemba 19, 2018 Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Flora Mtalania, amesema Mahakama  imeshindwa kuthibitisha makosa hayo baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili.

Amesema mlalamikaji ana haki ya kukata rufaa endapo hakuridhika na hukumu hiyo.

Awali,  akizungumza kabla ya kutolewa hukumu hiyo wakili wa Serikali, Raymond Kimbe amesema walikuwa tayari kwa hukumu hiyo huku wakili wa utetezi, Thomas Msasa akibainisha kuwa wana imani na Mahakama kuwa ni chombo cha kutoa haki.

Diwani huyo alidaiwa kutenda kosa hilo Aprili 12, 2018 na kwa mara ya kwanza alifikishwa mahakamani Mei 4, 2018.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )