Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, September 5, 2018

Baraka Da Prince Amwangukia Mange Kimambi

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo mwenye 'hit song' ya 'sina', Baraka The Prince amemuomba msamaha mwanadada mkosoaji wa mtandaoni, Mange Kimambi asimuhusishe katika 'vichambo' anavyovitoa, kwa madai ana hofia kuharibiwa kipaji chake.

Baraka ametoa kauli hiyo leo asubuhi kupitia ukurasa wake wa Instagram Septemba 05, 2018, baada ya kupita saa chache tokea Mange Kimambi kuuaminisha umma kuwa Wema Sepetu alishawahi kutoka kimapenzi na kijana huyo lakini suala hilo amekuwa akilificha

Mange ametoa madai hayo wakati alipokuwa anaendelea 'kuchambana' na Wema Sepetu, katika ugomvi uliozunguka mitandaoni unahusisha imani za kishirikina ambapo mrimbwende huyo anadaiwa kuwa kinara wa matukio hayo pamoja na kuongoza idadi kubwa ya kulala na wanaume waliokuwa maarufu na wasiokuwa na majina makubwa ndani na nje ya nchi.

"Kwanza niseme samahanini sana kwa kinachoendelea katika 'page' ya Mange kimambi, ningeomba nisemehe kitu kimoja na kikufike dada yangu Mange kuwa najenga 'brand' yangu katika mazingira magumu sana, natukanwa, nadharaulika, nakatishwa tamaa. Lakini 'stil' naamini katika ubora wa kile nachokifanya ndio kitanifanya niendelee kutetea nafasi hii niliyonayo", ameandika Baraka.

Pamoja na hayo, Baraka ameendelea kwa kufafanua baadhi ya mambo kuwa "nimeshatengenezewa stori nyingi mbaya ili kusudi nishuke na kupotea kabisa, basi naomba na wewe Mange usiwe miongoni mwa wanaotaka kuiporomosha 'career' yangu na kama niliwahi kukukosea sehemu yeyote tafadhali nikuombe msamaha na hilo suala lako unalotaka kupotosha jamii kuhusu mimi uachane nalo".

Aidha, Baraka amedai hajawahi kuwa na ukaribu wa kupitiliza na Wema kwani ana mheshimu kama dada yake ambaye aliyeweza kumfahamu kupitia kazi zao za sanaa huku akimsisitiza Mange aachane na yeye juu ya jambo hilo alilo muhusisha.

"Naomba sana dada yangu nisamehe kwa hilo mimi sio mtu wa hizo 'trend' muziki na mashabiki ndio maisha yangu 'please', kama kuna mtu amekutuma mtalaaniwa wote", amesisitiza Baraka.

Mwanadada Mange Kimambi ambaye anaishi mjini Los Angels nchini Marekani amejipatia umaarufu mkubwa kwa harakati za kukosoa watu mbalimbali bila ya kuwa na hofu juu ya jambo lolote.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )