Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, September 1, 2018

Bobi Wine aruhusiwa kuondoka Uganda

Mbunge wa Uganda ambaye inadaiwa aliteswa na maafisa wa usalama, Robert Kyagulanyi  maarufu kwa jina la Bob Wine ameruhusiwa kusafiri kuelekea Marekani kwaajili ya matibabu.

Alhamisi usiku Polisi walimkamata Kyagulanyi na mbunge mwenzake wa upinzani Francis Zaake uwanja wa ndege wa Kampala wakati wakijiandaa kwenda nje ya nchi kupatiwa matibabu.

Polisi walidai kuwa viongozi hao wa upinzani, ambao wote wanakabiliwa na tuhuma za uhaini walikuwa katika harakati za kukimbia nchi.

Hata hivyo, wabunge hao wawili wamesema kuwa waliteswa baada ya kukamatwa huko nyuma na hospitali ya Kampala ilitoa pendekezo kwamba wapatiwe matibabu nje ya nchi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )