Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, September 12, 2018

CCM Wampitisha Zuberi Kuchauka wa CUF Kugombea Ubunge

Zuberi Kuchauka amepitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea ubunge Liwake katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Oktoba 12.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humprey Polepole imesema Kuchauka amepitishwa leo na Kamati Kuu ya CCM iliyokutana jijini Dodoma chini ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho  Zanzibar, Rais Dk Ali Mohamed Shein.

“Kikao cha Kamati Kuu Maalum pamoja na mambo mengine kimemteua Zuberi Mohamed Kuchauka kuwa mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Liwale,” amesema Polepole.

Amesema pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu imeiagiza Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kushughulika na utatuzi wa shida za watu sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

“Kikao pia kimewapongeza wanachama wa CCM na wananchi hasa katika maeneo yenye uchaguzi mdogo kwa utulivu, mshikamano na kushiriki  kutumia haki yao ya kisiasa kuchagua viongozi wao katika ngazi ya majimbo
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )