Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, September 28, 2018

CHADEMA Wataja Sababu za Kutohudhuria Uzinduzi wa Flyover ya TAZARA

CHADEMA wameibuka na kutoa sababu za Wabunge wake kutofika katika shughuli ya uzinduzi wa barabara ya juu 'Flyover' katika eneo la Tazara jijini Dar es salaam iliyofanywa na Rais Magufuli.

Wabunge wa upinzani kupitia CHADEMA jijini Dar es salaam ni John Mnyika wa Kibamba, Halima Mdee wa jimbo la Kawe pamoja na Saed Kubenea wa Ubungo.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, amesema,  sababu zilizowafanya Wabunge wa Kawe Halima Mdee na wa Kibamba John Mnyika kutokufika katika uzinduzi uliofanyika jana ni  kwa sababu walikuwa na kesi katika Mahakama ya Kisutu.

“Tumemsikia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisema Wabunge wa CHADEMA walialikwa kwenye uUzinduzi huo na hawakufika, walikuwa Mahakamani wakati shughuli zikiendelea , hivyo wasingeweza kuwa Mahakamani na wakati huohuo wakahudhuria”, amesema Mrema.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )