Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, September 22, 2018

Diamond Amuunga Mkono Jokate....Aahidi Kukamilisha Madarasa Matatu Kisalawe

Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz ni miongoni mwa waliojitolea kuinua elimu ya watoto katika Wilaya ya Kisarawe ambayo inaongozwa na Jokate Mwegelo.

Muimbaji huyo ameahidi kukamilisha ujenzi wa madarasa matatu kwa upande wa madirisha na milango. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

"Kwa kutambua thamani ya Elimu kwa watoto na wadogo zetu........Kwa kumuunga mkono Mh Rais John Pombe Magufuli katika kuhakikisha watoto wetu wa Tanzania wanapata elimu Bora na Bure. Na kumuunga mkono Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mh Jokate Mwegelo Katika kampeni ya kutokomeza Zero Kisarawe." ameeleza.

"Mimi Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz Naahidi kuchangia madirisha na milango kwa Madarasa Matatu, kwa ajili ya Shule Kisarawe. tafadhali tuwasaidie watoto au wadogo zetu kwa Kisarawe kwa kuchangia kupitia maelekezo yalio kwa clip hii ama, kufika pia Tarehe 22/09/2018 pale Minaki Sekondari kwenye Harambee ya Kuchangia Kampeni Hii ya Tokomeza Zero," ameeleza Diamond.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )