Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, September 20, 2018

Fedha ya Zambia kuanza kutumika Tanzania

adv1
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga na mwenzake wa Benki Kuu ya Zambia, Dk. Denny Kalyalya, wanatarajia kutia saini makubaliano ya kuruhusu matumizi ya fedha za nchi mbili shilingi ya Tanzania na Kwacha ya Zambia ziweze kutumika katika nchi hizo mbili hasa katika eneo la mpakani la Tunduma na Nakonde.

Hatua hiyo sasa inakwenda kutoa fursa ya kiuchumi kwa kufanya biashara na uwekezaji katika miji ya mpakani ya Tunduma (Tanzania) na Nakonde (Zambia).

Makubaliano hayo yanatarajiwa kusainiwa kesho mkoani Songwe mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa huo, Brigedia Jenerali Nicodemas Mwangela na baada ya tukio hilo utafanyika mkutano wa hadhara katika eneo la Tunduma ambapo magavana hao watazunguza na wananchi wa pande zote mbili.

Taarifa iliyotolewa  na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ilieleza kwamba lengo la makubaliano hayo ni kuwezesha kupokelewa sarafu za nchi hizo mbili na taasisi rasmi za fedha ikiwa ni pamoja na mabenki ya biashara ya pande zote mbili bila kikwazo chochote.

“Nia ya hatua hii ni kurahisisha biashara kati ya nchi hizi mbili, kuondoa biashara holela ya fedha za kigeni mpakani na kuziwezesha serikali za Tanzania na Zambia kujipatia mapato stahiki ya kodi na tozo kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazofanyika katika miji hiyo.

“Benki Kuu za mataifa haya mawili rafiki, zimefikia hatua ya kusaini makubaliano hayo baada ya utafiti na majadiliano yaliyoanza tangu mwaka jana ambayo yalikuwa na lengo la kupambana na biashara holela ya fedha za kigeni na kuwawezesha wananchi wa pande zote kunufaika na shughuli za kiuchumi za mpakani,” ilieleza taarifa hiyo.adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )