Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, September 3, 2018

Jambazi Lanaswa na Jeneza Songwe

Jeshi la Polisi Mkoani Songwe, linamshikilia mtu mmoja ambaye amekuwa akijihusisha na matukio mbalimbali ikiwemo, ujambazi, utapeli kwa kutumia nembo za freemason, akiwa na silaha aina ya  Air Gun  pamoja na risasi 135.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi Mathias Nyange amesema, mtuhumiwa huyo aliyejulikana kwa jina la Jerico Chifunda Msukuma, ni mkazi Nazareti Mjini Tunduma.

Mbali na kukutwa na vitu hivyo pia amekutwa na vitambulisho vinavyoonesha uraia wa nchi mbili Tanzania na Zambia ambapo anadaiwa kufanya matukio ya uhalifu kisha kukimbilia nchini Zambia.

Vitu vingine ambavyo amekutwa navyo Msukuma ni pamoja na jeneza dogo, pingu,  pasi inayotumika kutapeli watu kupata fedha, mashine ya kunakilisha  noti bandia, na karatasi zinazolingana ukubwa na noti ya shilingi 10,000.

Katika Hatua nyingine jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watu 12 wakiwa na vitu mbalimbali kama runinga na radio, ambavyo vimeibwa katika matukio mbalimbali  na kwamba tayari vimetambuliwa na wamiliki.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )