Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, September 22, 2018

Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally atuma salamu za rambirambi ajali ya MV Nyerere

adv1
Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally ametuma salamu za rambirambi kwa Rais John Magufuli na Watanzania kutokana na ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi Septemba 20, 2018 Kisiwa cha Ukara, wilayani Ukerewe Mkoa wa Mwanza.

Ametuma salamu hizo leo Jumamosi Septemba 22, 2018 akiwa mkoani Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi, kulazimika kubadili ratiba ya ziara hiyo.

“Taifa letu lipo kwenye msiba na kama mnavyojua bendera zinapepea nusu mlingoti. Tuendelee kuwaombea na tutafakari namna tunavyoweza kukabiliana na majanga yanayotokea,”amesema Dk Bashiru.

“Tupate fursa ya kutafakari na kujadiliana namna nzuri ya kusimamia vyombo vyetu vya usafiri na shughuli zote zinazohusu huduma kwa Watanzania.”

Amesema kutokana na ajali hiyo amelazimika kubadili ratiba ya ziara yake na kuungana na Watanzania wengine katika maombolezo.

 “Sijasitisha  ziara yangu lakini itabidi baadhi ya ratiba zirekebishwe ziendane na maombolezo,” amesema.

“Nimewatuma wajumbe wawili Humphrey Polepole (Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM) na  Kanali Lubinga (Ngemela-Katibu wa Siasa na Uhuasiano wa Kimataifa wa CCM) kwenda kule wafuatilie  namna shughuli zinavyoedelea.”
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )