Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, September 20, 2018

Kivuko Cha Mv. Nyerere Kinachotoa Huduma Kati Ya Ukara Na Bugolora Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza Kimezama Leo Majira Ya Mchana

adv1
Kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari kati Bugorora katika Kisiwa cha Ukerewe na Kisiwa cha Ukara katika Ziwa Victoria mkoani Mwanza kimezama leo Alhamisi Septemba 20, 2018.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara.

Kamanda Shana amesema kuwa kivuko hicho kimezama leo mchana  baada ya kupinduka.

“Kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa nane kamili mchana kilipinduka,” amesema.

Amesema kuwa watu watatu wameokolewa na shughuli ya uokoaji inaendelea ikiongozwa na mkuu wa mkoa huo, John Mongella.

Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )