Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, September 1, 2018

Lulu Diva Azungumzia nyimbo Mbili Mpya za Rich Mavoko

Msanii wa muziki Bongo, Lulu Diva amefunguka kuhusu nyimbo mbili mpya za Rich Mavoko, Happy na Ndegele.

Muimbaji huyo akipiga stori na SnS Tanzania (Simulizi na Sauti) amesema kuwa anaona nyimbo hizo zinafanya vizuri tu mtaani.
 
"Ngoma bado zinazidi kwenda na bado muda, ngoma zinazidi kusikilizwa sio kwamba hazijafanya vizuri, mimi napita mtaani nazisikia," amesema Lulu Diva.

Alipoulizwa anahisi kwanini Rich Mavoko hajazifanyia nyimbo hizo promotion kwenye media, alijibu, 'Lakini nafikiria na yeye mwenyewe ametoa kama bonus, unaona hajafanya interview yoyote, hajaongelea popote, ametoa tu,'.

Wimbo wa mwisho kwa Lulu Diva kutoa amemshirikisha Rich Mavoko unaokwenda kwa jina la Ona ambao hadi sasa una views zaidi ya Milioni 1 katika mtandao wa YouTube na ndio wimbo wa kwanza kwa msanii huyo kufanya hivyo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )