Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, September 1, 2018

Makonda: Ninalaani tukio la kushambuliwa raia kisa 50,000 ya usafi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameagiza mgambo waliopiga raia katika eneo la Bunju A kuchukuliwa hatua kali kwani walichokifanya haukuwa mpango wa mkoa.

Makonda amekemea vikali kitendo hicho amabacho kimefanyika kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Bunju ambapo Mgambo hao wamepiga raia na kuwajeruhi akiwemo mfanyabiashara, Robson Orotho mkazi wa Bunju kutokana na kushindwa kulipa Sh. 50,000 ya taka.

”Nimeshtuka sana baada ya kuona video hiyo sio kitendo cha kufanywa na watendaji kwani lengo letu ni kusimamia usafi na si kupiga raia, nalaani kitendo hicho na naagiza hatua kali zichukuliwe dhidi yao,” amesema Makonda.

Kwa upande wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni limethibitisha kuwashikilia mgambo watatu wa Manispaa hiyo ambao wamehusika katika tukio hilo na taratibu za kisheria zinaendelea na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Aidha, Kamanda Murilo amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Goodluck Festo, Rehema Nyange na Kelvin Edson, ambao wote ni Mgambo wa Manispaa hiyo huku akibainisha kuwa mfanyabiashara huyo anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mwananyamala.

Siku za hivi karibuni zimesambaa picha za video katika mitandao ya kijamii zikionyesha mgambo wakitoa kipigo kwa watu na kuzua taharuki, wengi wakiwa ni wafanyabiashara ndogo ndogo
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )