Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, September 1, 2018

Makontena ya Makonda kupigwa tena mnada leo

Makontena 20  yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ‘kwa ajili ya ofisi za walimu’, yanapigwa mnada kwa mara ya pili leo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Jumamosi iliyopita, makontena hayo yalipigwa mnada lakini yalikosa wateja kutokana na wengi kushindwa kufikia bei iliyokuwa ikiuzwa ya Sh. milioni 60 kwa kontena moja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali Yono Action Mart, inayosimamia mnada huo, Scollarstika Kevela jana alisema mnada huo unaorudiwa kwa mara ya pili utafanyika kuanzia saa 3:00 bandarini eneo la Kurasini.

“Mnada huu utafanyika tena kesho (leo) na makontena yale yale 20 tutayanadi kwa wateja ingawa sijui kama yameongezeka kwa sababu TRA ndio wasimamizi wa mnada huu,” alisema Kevela.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )