Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, September 15, 2018

Makontena ya Makonda Yakosa Wateja Tena

Makontena  ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam leo Jumamosi Septemba 15, 2018 yamekosa tena wateja.

Makontena hayo yameshindikana kuuzwa katika mnada uliofanyika jijini Dar es Salaam. Hii inakuwa ni mara ya nne makontena hayo kushindwa kuuzika.

Akizungumza kwenye mnada huo, mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya udalali ya Yono, Scolastica Kevela amesema mnada huo umeendeshwa lakini mnunuzi hajapatikana.

Kevela amesema hadi sasa bei zinazofikiwa na wateja hazijafikia malengo waliyowekewa. Amesema wao kama madalali wataendelea kufanya utafiti wa kuwapata wateja.

Wateja wachache waliokuwa kwenye mnada huo walionekana kutaja bei lakini hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kufikia kiwango kilichowekwa.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )