Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, September 6, 2018

Mali za Mbunge wa Geita Mjini, Joseph Kasheku(Musukuma) kupigwa mnada

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kupitia kampuni ya udalali ya LJ International Ltd imetangaza kuzipiga mnada mali za Mbunge wa Geita Mjini, Joseph Kasheku maarufu kama Musukuma.

Mali zilizotajwa kupigwa mnada ni pamoja na kiwanja Na.275 Block kilichopo Mbezi Dar es Salaam na kiwanja Na.’2’ block ‘A’kilichopo Korogwe mjini.

Mali nyingine ni shamba Na.201 liliolopo kijiji cha Igate Mkoani Geita, kiwanja Na. 116 block A Buswelu Kaskazini na kiwanja Na. 48 block T katikati ya jiji la Mwanza.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya NBC, William Kalage amesema ni kweli mali hizo zinapigwa mnada. Musukuma hakupatikana kuzungumzia suala hilo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )