Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, September 6, 2018

Marwa Ryoba: “Rais Magufuli Nipo tayari kuacha Ubunge, Sisi WanaCHADEMA ni wako”

Mbunge wa Serengeti (Chadema) Marwa Ryoba amesema yupo tayari kuacha ubunge ili awape wananchi waliomchagua barabara ya lami.

Akizungumza leo Septemba 6, 2018 katika ziara ya Rais John Magufuli wilayani Serengeti,  Ryoba amesema wilaya hiyo haijanufaika na Hifadhi ya Serengeti kutokana na kukosekana kwa barabara ya lami.

Amesema ingawa yupo Chadema lakini anampenda Rais Magufuli.

“Mimi nipo tayari hata kuacha ubunge lakini unipe barabara, WanaCHADEMA wote sisi ni wa kwako, vyama vyote vya upinzani sisi ni wa kwako usitutupe Rais, tupo chini ya magoti yako” -Mbunge wa Serengeti Chacha Marwa akiongea mbele ya Rais Magufuli

Mbunge huyo amemshukia mkurugenzi wa mji wa Serengeti, Juma Hamsini akidai kuwa amefuja zaidi ya Sh500 milioni.

Kwa upande wake, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imetenga Sh 11.2 bilioni ili kutatua tatizo la maji Mugumu.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )