Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, September 26, 2018

Mbatia Agoma Kuhudhuria Uzinduzi Flyover Tazara.....Adai Mwaliko wa Makonda Haujafuata Taratibu


Wakati Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho akitarajiwa kuzindua matumizi ya barabara ya juu (Flyover) Tazara viongozi mbalimbali walipewa mualiko na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akiwemo Freeman Mbowe, Halima Mdee, pamoja na James Mbatia kushiriki tukio hilo.

Mbatia alipotafutwa ili kufahamu kama angeitikia wito wa mkuu huyo wa mkoa Mbatia amesema anapenda maendeleo lakini kiongozi huyo alipaswa kufata taratibu kutoa mwaliko kwa viongozi hao.

“Yaani kweli mimi Mbatia nialikwe na Mkuu wa Mkoa (Makonda) kupitia vyombo vya habari sio sawa kabisa, hatukatai maendeleo lakini alipaswa kufata taratibu kabla za kunialika kwa kunitumia barua sio kutumia vyombo vya habari. ”, amesema Mbatia

Mapema jana katika mkutano wake za kifedha Makonda aliwaalika baadhi ya wabunge wa Upinzani ili kuhudhuria tukio hilo ambalo linatajwa kupunguza adha ya foleni kwa watumiaji wa barabara ya Mandela a Nyerere na kusaidia kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 400.

“Ningependa kuona viongozi wa vyama vyote waje, akiwemo Mbatia, Mbowe, Zitto Kabwe na Halima Mdee wasisusie kama ilivyo mambo ya uchaguzi, nawaalika vyama vyote vya siasa mimi nitakuwa mwenyeji wao na tutawawekea viti ” alisema Makonda
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )