Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, September 18, 2018

Mboto: Hakuna Msanii Wakuliziba Pengo la Mzee Majuto

adv1
Mchekeshaji mahiri Bongo, Haji Salum ‘Mboto’ amesema watu wasipoteze muda wao kufikiria kuna msanii atakayeweza kuziba pengo la mchekeshaji nguli Bongo, marehemu Amri Athumani ‘King Majuto’, akisisitiza hilo haliwezekani na kuongeza hata leo yeye akifariki dunia hakuna wa kuziba pengo la Mboto.

“Ukweli King Majuto ni yeye na mimi ni mimi niliona wakati alipofariki dunia Kanumba, walikuja wanaofanana naye lakini si wasanii na wote waliotaka kutembelea nyota ya Kanumba wamepotea,” alisema Mboto.

Mboto anasema jambo la muhimu ni kuenzi mazuri ya King Majuto kwa kufanya vizuri katika tasnia ya filamu na vichekesho na si kufanana na kumwiga msanii mwingine. 

Anasema sanaa ni ubunifu kama yeye pamoja kuwa ni Mzaramo lakini watu wanaamini ni Mkongo kwa jinsi anavyoigiza sauti za Kikongo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )