Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, September 19, 2018

Mbowe Agoma Kuachia Uenyekitri CHADEMA

adv1
Mwenyekiti  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe,  amesema kamwe hatoachia kiti hicho kwa kusikiliza maneno ya watu wa nje ya chama ambao hata hawakumchagua.

Mbowe amesema hayo leo Septemba 19, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Amesema chama hicho kufanya vibaya sababu si yeye, “Na mimi niliwekwa na wanachama, wakitaka wataniondoa lakini siondoki kwa kelele za watu.”

Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema kamwe hatakuja kukipigia magoti chama tawala cha CCM.

Amesema hata siku moja CCM haitafurahi kumuona anakuwa na nguvu kwenye chama, lengo lao ni kuona anakuwa dhaifu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )