Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, September 9, 2018

Mbunge CCM Amvaa Lowassa Sakata la Richmond

Mbunge wa Ulanga (CCM),Goodluck Mlinga amewataka wakazi wa Monduli mkoani Arusha kumuuliza waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa sababu za kujiuzulu baada ya kuibuka kwa sakata la  Richmond.

Mlinga alitoa kauli hiyo jana Jumamosi Septemba 8, 2018 katika mkutano wa kampeni jimbo la Monduli uliofanyika eneo la Mukuyuni.

Alisema Lowassa anamshambulia mgombea wa CCM katika jimbo hilo, Julius Kalanga kuwa amejiuzulu uanachama wa Chadema na kuhamia chama tawala kwa sababu alikuwa na deni la Sh. milioni 600, wakati yeye alijiuzulu uwaziri mkuu kwa kuchukua fedha za Richmond.

Waziri huyo mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, amekuwa hazungumzii sakata hilo la Richmond na inapotokea kulizungumzia amekuwa akieleza kuwa alijiuzulu kisiasa kuilinda Serikali ya CCM na kwamba ushiriki wake ulitokana na maagizo kutoka juu.

Kampuni ya Richmond Development Company ya Marekani ilipewa zabuni ya kufua umeme wa dharura wakati nchi ilipokuwa na tatizo kubwa la ukosefu wa nishati hiyo mwaka 2006.

“Jamani kati ya anayedaiwa na ambaye amejiuzulu kwa tuhuma za kuchukua fedha za umma nani bora,” alihoji Mlinga.

Mlinga alisema watu wengi wamekopa na kudaiwa lakini sio tatizo kwa kuwa anayekopa hulipa, deni halifungi mtu.

Aliwataka wakazi wa Monduli kupuuza tuhuma kuwa Kalanga alijiuzulu ili kulipiwa deni kwani kauli hizo ni za kisiasa.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )