Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, September 11, 2018

Mgambo wa Makonda Waingiza Milioni 346 Kwa Mwezi

Baada ya kuendesha kampeni ya usafi kwa mwezi mmoja, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda ametoa taarifa ya kampeni hiyo.

Akizungumza jana katika kikao hicho Makonda alisema kuwa tangu kuanza kwa kampeni hiyo zaidi ya watu 10000 wamekamatwa, watu 4443 waliachiwa huru, 376 walipata dhamana na takribani watu 6577 walilipa faini iliyofikia shilingi milioni 346 na laki 6 ambapo nusu ya fedha hizo ilikuwa ni malipo kwa mgambo wanaosimamia usafi na hadi sasa watu 6 bado wapo mahakamani.

Aidha amesema kuwa yeye na wakuu wa Wilaya wamelaani kitendo cha mgambo wa kusimamia usafi kumpiga raia katika eneo la Bunju na wamefatilia na hadi sasa watuhumiwa wapo katika gereza la Segerea na amewataka mgambo hao kufanya kazi kwa kufuata na kusimamia sheria kwani hakuna sheria inayorusu kupiga raia.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )