Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, September 8, 2018

Mgambo wa Makonda wanaodaiwa kupiga raia wapandishwa kizimbani, Wanyimwa Dhamana

Askari Mgambo wawili na Afisa mtendaji wa kata ya Bunju,
wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kumjeruhi kwa kutumia Rungu mkazi wa Bunju Robinson Olotho.

Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono amewataja washtakiwa hao kuwa ni askari Mgambo Kelvin Sawala (25) na Goodluck Tarimo (30) ambao wanashtakiwa pamoja na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bunju Ibrahim Mabewa (39).

Wakisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde imedaiwa August 30, 2018 huko  Bunju Wilayani Kinondoni, washtakiwa hao walimpiga Olotho kwa kutumia rungu sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha makali

Hata hivyo washtakiwa wamekana kosa hilo na wamerudishwa rumande baada ya wakili wa serikali, Nassoro Katuga kuieleza mahakama kuwa, licha ya kesi hiyo kudhaminika lakini wanaiomba mahakama isubirishe dhamana ya washtakiwa hao kwa sababu kuu mbili.

Alizitaja sababu hizo  kuwa kuna suala la kiusalama ambapo washtakiwa walionekana kwenye video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, hivyo kama watapatiwa dhamana usalama wao utakuwa shakani kwa sababu wananchi na ndugu wa mjeruhiwa watakuwa na hasira.

Pia akadai sababu nyingine ni kwamba mjeruhiwa bado yupo hospitali na hali yake ya kiafya sio nzuri.

Hakimu Kasonde alipowauliza washtakiwa hao kuhusu hoja hizo walidai hali ya afya ya mjeruhiwa walionana naye jana na anaendelea vizuri wala hayupo hospitalini na kuwa suala la usalama wao liko vizuri, hivyo wanaomba dhamana,

Hata hivyo, Hakimu Kasonde alisema mahakama imekubali hoja za upande wa mashtaka kuhusu usalama wa washtakiwa hao, hivyo wananyimwa dhamana hadi hapo itakapojiridhisha kuhusu usalama wao.

Upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi September 20,2018.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )