Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, September 14, 2018

Mkurugenzi Halmashauri ya Msalala Apata Ajali

adv1
Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala,  Simon Belege na mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mibako Mabubu wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wamepanda kugonga ng’ombe katika mteremko wa Mlima Sakenke.

Viongozi hao walikuwa wakitokea mkoani Dodoma kuelekea Igunga, Tabora kuwahi kikao cha utekelezaji wa ilani ya CCM kitakachofanyika kesho Jumamosi Septemba 15, 2018.

Katika gari hilo, Mkurugenzi huyo  alikuwa pamoja na mwenyekiti wa halmashauri hiyo, mweka hazina, Masatu Mnyoro na mwanasheria wake, Mashaka Mabula.

Majeruhi wa ajli hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Igunga mkani Tabora wakiendelea kupatiwa matibabu.
 
Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Bonaventura Kalumbete amesema  Belege na Mabula ndiyo waliokuwa wamelazwa lakini baada ya kuwapatia matibabu hali zao zinaendelea vizuri na wakati wowote wataruhusiwa.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )