Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, September 13, 2018

Ommy Dimpozi Kaweka Picha Akiwa ICU na Kuandika Ujumbe Mzito wa Hisia

Kwa mara ya kwanza msanii Ommy Dimpoz amechapisha ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram tangu alipoanza kupatiwa matibabu Afrika Kusini.

Leo September 13, 2018  ni siku ya kuzaliwa kwa msanii huyo, ambapo ameandika  ujumbe mrefu kwa mashabiki wake, watu wake wa karibu na Management yake kwa kuwa naye kwa kipindi chote. 

Chini ni kile alichoandika Ommy Dimpoz.

Leo 13th September ni kumbukumbu yangu ya siku ya kuzaliwa.
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu (ALHAMDULILAAH) kwa kunipa nafasi ya kuuona mwaka mwingine, kwani niliyoyapitia katika kipindi cha takribani miezi 5 kama ingekuwa sio mapenzi yake yeye (M/Mungu) basi ingekuwa imebaki history.

Nilichojifunza kipindi hichi chote ni kuwa kuumwa ni Ibada na sisi kama binadamu hatujakamilika leo unaweza kuwa mzima na kesho ukawa mahututi kitandani, ndio maana nimeamua kushare picha ambayo nilipigwa nikiwa ICU japo nafahamu sio kitu kizuri kupost picha kama hii kwenye mitandao ila nia yangu ni kujaribu kukumbushana sisi kama Binadamu kuwa kuna leo na kesho kwahiyo tusiishi kwa chuki na Uadui maana hatujui kesho yetu itakuwaje!!

Kuna kipindi wakati nimelazwa nilikata tamaa ya kuishi nikaona labda muda wangu umekwisha lakini hapo Hospital akaletwa mgonjwa mwingine ambae alikuwa pembeni yangu alishambuliwa na majambazi kwa risasi tisa mwilini lakini madaktari wakafanikiwa kuokoa maisha yake na akapona so nikajiuliza mimi ni nani nikate tamaa ya kuishi na nikajifunza kwamba kuugua sio kufa.

Ni vyema tukipata nafasi basi tuwaombee na kuwafariji wagonjwa kwani wanayoyapitia ni magumu mno. Kwasasa namshukuru Mwenyezi Mungu naendelea vizuri na bado niko kwenye recovering, pia nawashukuru watu wote ambao mmekuwa mkiniombea dua nipone kwa haraka kuanzia mashabiki mpaka wasanii wenzangu na kila mtu aliyeniombea kwa imani yake Nashukuru sana. Mungu awabariki sana.

Pia Shukran za dhati kwa Familia yangu, Marafiki zangu wa Karibu, Management yangu ROCKSTAR FAMILY @officialalikiba na my lovely Manager @sevenmosha ambaye amehangaika na mimi mfano wa Mama Mzazi na mtoto wake pamoja na my Big Brother Governor @joho_001 ambaye ameniuguza kwa kipindi hichi chote chini ya uangalizi wake na Madaktari kuanzia Kenya Mpaka South Africa.

ASANTENI SANA NA INSHAALLAAH KWA UWEZO WA ALLAAH I WILL COME BACK STRONGER 💪🏽🙏❤

Tangu mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu Ommy Dimponz alikuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini ambapo alifanyiwa upasuaji wa koo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )