Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, September 23, 2018

Oparesheni Tokomeza ZERO Ya DC Jokate Mwegelo Yapata Milioni 125

adv1
Jana September 22, 2018 ndio ilikuwa harambee ya kuchangia Programu iliyoanzishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kwa ajili ya kutokomeza Zero.

Program hiyo imelenga kuinua kiwango cha ufaulu wilayani humo kwa kuhakika wanafunzi wanakuwa na madarasa mazuri ya kusomea, vifaa na chakula. 

==>.Soma taarifa kamili ya Jokate Mwegelo hapo chini;

Kutokana Na Maombolezo Ya Msiba Ukerewe, Serikali ya Wilaya ya Kisarawe kwa pamoja tuliamua kuhairisha shamrashamra za programu yetu ya Tokomeza Zero Harambee Pale Minaki Sekondari, tukasimama na kuombea ndugu zetu waliopoteza maisha lakini pia kutoa faraja kwa kuchangia Milioni Moja kama rambirambi kutoka Wilaya ya Kisarawe. .

Lakini tuliruhusu waliofika kuchangia na baada ya kupiga mahesabu leo tumeweza kuchangisha Milioni 125.062 katika awamu hii ya kwanza. Hii ahadi ya michango ya pesa taslimu imevuka lengo letu la awali ambalo lililuwa ni Milioni 100 ilituweze kuhudumia makambi ya wanafunzi mpaka mwezi wa kumi na moja ambapo wataanza mitihani yao ya mwisho ya taifa. .

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana wananchi wenyeji wa Kisarawe kwa kuitikia wito kwa wingi sana ila pia na wadau wetu kutoka nje ya Kisarawe. Tunawashukuru sana. Mungu awaongezee pale mlipopunguza. .

Kwa kipekee nimshukuru Ndg. Masanja Kadogosa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika La Reli Tanzania (TRC) na Wakandarasi Yepi Merkezi kwa kuahidi kujenga madarasa wenyewe na kuchangia chakula kwenye makambi yetu. Reli ya Kisasa inayojengwa inapita Kisarawe na tunawezesha ujenzi huu kwa ku-supply malighafi za ujenzi. Kwahiyo Kisarawe ni wadau wakubwa wa TRC. .

Naendelea kuwakaribisha wadau mbalimbali kutuunga mkono kwenye Programu hii ya Tokomeza Zero awamu zinazofuata ni kuboresha mazingira ya kusoma na kufundisha ikiwa ni kuhakikisha miundombinu mbalimbali ya Elimu inapatikana. Na pia tutakuwa na Tokomeza Zero Inspirational Talks - kufuata wanafunzi na jamii walipo na kuongea nao juu ya umuhimu wa Elimu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )