Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, September 8, 2018

Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi.....“Nimeshtuka watu 11 kufariki tena kwa ajali mkoani Mbeya”

“Nimepokea kwa mshtuko taarifa ya vifo vya watu 11 vilivyotokea leo jioni huko Mbeya, kwa mara nyingine tumewapoteza Watanzania wenzetu katika ajali ya barabarani na wengine wameumia, nimesitishwa sana na vifo hivi.
 
“Nawapa pole wanafamilia wote waliopoteza ndugu zao katika ajali hii na pia nawapa pole majeruhi wote, nawaombea watibiwe na kupona haraka ili waweze kuungana na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku”

Ni salamu za rambirambi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alizozitoa kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila kufuatia ajali ya barabara iliyosababisha vifo vya watu 11 na wengine 15 kujeruhiwa.

Ajali hiyo imetokea  jana katika mteremko wa mlima wa Igawilo Jijini Mbeya baada ya Lori lililokuwa na shehena ya viazi, likitokea Tukuyu kwenda Mbeya Mjini kuyagonga magari matano likiwemo basi dogo lililokuwa na abiria.

Pamoja na kutoa pole kwa wafiwa wote, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na vifo hivyo Rais Magufuli amewaombea Marehemu wote wapumzike mahali pema peponi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )