Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, September 21, 2018

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Atuma Salamu za Rambirambi Ajali ya MV Nyerere...Kasema Kenya Ipo Tayari Kutoa Msaada Wowote Utakaohitajika

RAIS  wa  Kenya Uhuru Kenyatta , ametuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu  zaidi ya 100 waliofariki mpaka sasa kutokana na kivuko cha MV.Nyerere kupinduka Ziwa Victoria tarehe 20 Septemba 2018

Katika ujumbe wake alioutuma katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Kenyatta ametoa pole kwa Watanzania kufuatia ajali hiyo.

“Kwa niaba yangu na  wananchi wa Kenya, natuma salamu za rambirambi kwa ndugu yangu  Rais Magufuli pamoja na  majirani zetu raia wa Tanzania katika kipindi hiki kigumu kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama Ziwa Victoria. ” amesema.

Rais Kenyatta amesema serikali yake ipo tayari kutoa msaada wowote utakaohitajika  kufuatia ajali hiyo.


Kivuko hicho kilizama jana mchana Septemba 20, 2018 na hadi leo  Septemba 21, 2018 maiti za watu 100 zimeopolewa.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )