Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, September 6, 2018

Serikali Yakanusha....Yasema Hakuna Tishio Lolote la Sunami Katika Bahari ya Hindi

Serikali kupitia Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu imesema hakuna tishio lolote la Sunami katika Bahari ya Hindi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jioni Septemba 5,2018, Mkurugenzi wa idara hiyo, Kanali Jimmy Said alisema, Taarifa ya Sunami inayosambaa mitandaoni si ya kweli.

Alisema walikuwa wanafanya mazoezi ya utayari kwa magari ya zimamoto na watu wa hatua mbalimbali wakichukua.

“Taarifa za Sunami zinapotolewa wananchi hawachukulii uzito hivyo leo tulikuwa tunaangalia kama wananchi watalichukuliaje hili jambo,” alisema Kanali Said.

Alisema wamejipima mambo mengi na kwamba kama kungekuwa na tishio hilo kituo cha mawasiliano na dharura kilichopo chini ya Waziri Mkuu idara ya maafa ndiyo inaratibu kutoa taarifa ya Sunami.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )