Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, September 3, 2018

Serikali Yawataka Wananchi Kutonunua Sukari Inayouzwa Kwa Magendo maana ni Hatari kwa Afya Zao

Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba amewataka watanzania kuwa waangalifu na kuacha mara moja kununua sukari kutoka kwa wafanyabiashara na vifungashio holela, kwani hali hiyo ina hatarisha maisha yao pamoja na kuathiri uchumi wa nchi.
 
Dkt. Tizeba ametoa kauli hiyo baada ya bodi ya sukari kubaini uwepo wa kiasi kikubwa cha sukari kinachoingizwa nchini kimagendo, ikiwemo sukari nyeupe kwa ajili ya matumizi ya viwandani maarufu kama 'white sugar'.

"Sukari iliyokuwa kwenye vifungashio vya plastiki ambavyo havijulikani vimetoka wapi licha ya kwa muonekano wa macho ni sukari. Kifungashio kinapaswa kiwe na 'information' yote ya nani kafungasha, kilichomo humo ni kitu gani", amesema Dkt. Tizeba.

Pamoja na hayo, Dkt. Tizeba ameendelea kwa kusema "kwa kweli wananchi nawaomba muepukane na jambo kama hili la kununua sukari bila ya kusoma maelezo ya kwenye mifuko inayoelezea bidhaa husika kwasababu mnaweza kutumia sumu bila ya kujijua".

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Sukari nchini Bw. Miraji Kipande amesema katika operesheni hiyo wanayoendesha hadi sasa wameshakamata zaidi ya mifuko elfu nne na kufanikiwa kumkamata mfanyabiashara mmoja eneo la Tandika Jijini Dar es Salaam kwa kutengeneza vifunganishio 'fake'.

Katika miezi ya hivi karibuni hii ni mara ya pili kwa Waziri wa Kilimo Dkt. Tizeba kubaini uingizwaji wa bidhaa hiyo kimagendo na kutoa agizo kwa Jeshi la Polisi kuwakamata wahusika kwa kuwa vitendo hivyo ni kinyume za sheria za nchi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )