Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, September 24, 2018

Soudy Brown Ashitakiwa Kwa Kosa la Kurusha Maudhui Mtandaoni Bila Kusajiliwa....Arudishwa Cetral Polisi

Kesi inayomkabili mtangazaji wa Clouds Media Soudy Brown, leo imesikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala akisaidiana na Wakili Maghimbi.

Katika maelezo ya awali Soudy Brown anashtakiwa kwa kosa la kurusha maudhui kupitia akaunti yenye jina la Shilawadu ambayo haijasajiliwa

Baada ya Hakimu kusikiliza kesi hiyo upande wa utetezi umeomba mshtakiwa apewe dhamana ambapo Hakimu amekubali hivyo mshtakiwa ametakiwa kuwa na mdhamini mmoja na bondi ya shilingi milioni 2, kesi hiyo imeahirishwa hadi Octoba 18, 2018.

Hata hivyo, Soudy Brown bado anashikiliwa na amerudishwa tena  polisi  Central kwa kuwa ana kesi nyingine ya kujibu inayomhusu yeye pamoja na Msanii Maua Sama ambaye hakuletwa mahakamani leo.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )