Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, September 23, 2018

Taarifa Toka Kurugenzi Ya Mawasiliano ya Rais IKULU

adv1
Rais John Magufuli amewapongeza askari wa usalama barabarani kwa juhudi zao za kusimamia usalama barabarani licha ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametoa pongezi hizo leo Jumapili Septemba 23, 2018 alipokutana na kunywa chai na baadhi ya askari hao Ikulu jijini Dar es Salaam, ikiwa ni muda mfupi baada ya kutoka katika Ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay.

Taarifa ya Rais kukutana na askari hao wa kikosi cha usalama barabarani imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa.

“Ninawapongeza trafiki wote kwa kazi mnazofanya, nafahamu mnakabiliwa na changamoto nyingi, mnafanya kazi zenu kwenye jua na mvua, wakati mwingine mnakwazwa na watumia barabara lakini mnaendelea na kazi,” amesema Rais.

“Nataka kuwatia moyo chapeni kazi, wanaovunja sheria za barabarani wachukulieni hatua, msitishwe na mtu yeyote lakini na nyie msimuonee mtu yeyote.”

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )